Mwanamuziki Christian Bella amedai utakuwa unamkosea ukimwita yeye ni
msanii wa muziki wa bendi au msanii wa muziki wa bongofleva kwa kuwa
anafanya muziki wa aina nyingi.
Mkali huyo wa masauti ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nishike’,
ameiambia Bongo5 kuwa yeye ni mwanamuziki kwa kuwa anafanya vitu vingi
ndani ya muziki.
“Mimi ni msanii ninayefanya muziki ndani ya Tanzania, sio muziki wa
bongofleva, sio muziki wa dansi, sio msanii wa taarabu,” alisema Bella
“Mimi ni mwanamuziki, mimi ni mwanamuziki kwa ujumla, usiniseme mimi ni
Bella msanii wa muziki wa dansi au Bella msanii wa muziki wa bongofleva
au Bella msanii wa taarab au Bella msanii wa R&B, Christian Bella ni
mwanamuziki,”
Aliongeza “Mimi nafanya muziki kufurahisha kila mtu, nafanya muziki
kufurahisha wanahip hop, wana bongofleva, wana dansi,wana taarab ndio
maana mimi naitwa mwanamuziki,”
Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa makao wa
kula kwa ajili ya ujio wa studio yake pamoja na label ya kusimamia
wasanii.
CREDIT: BONGO5
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...