• Home
  • About

Aggrey Morris azungumza haya baada ya kurejea tena uwanjani


Beki wa kati wa timu ya Azam FC, Aggrey Morris amefurahi kurudi tena uwanjani baada ya kuumia goti na kukaa nje ya uwanja takribani miezi mitatu.

Morris ambaye aliumia akiwa na timu ya taifa ya Zanzibar amesema alikuwa akiumia kuwa nje wakati timu yake ilihitaji msaada wake.

Akiongea na mtandao wa timu hiyo, Aggrey Morris alisema, “Nafurahi sana kurejea dimbani tena, nilikuwa natamani sana kucheza, kuna muda nilikuwa naumia sana nilipokuwa naona timu yangu inahitaji msaada wangu na mimi pia nilikuwa natamani kuisaidia, sisi wachezaji tunapenda kucheza, nilihisi kuna kitu naweza kuisaidia timu yangu kwa hiyo nafurahia kurejea na najua nitatoa mchango kwa timu yangu.”
“Mimi nawaambia mashabiki waendelee kuwa nami, kwa sababu najua walimiss kwa kipindi kirefu na wamenivumilia kusema kweli na wamenisapoti kwa kipindi chote kigumu pia watarajie tu kujitoa kwa moyo wangu wote kuisaidia timu yangu,” alimalizia Morris,” aliongezea Morris.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...