Unaweza kudhani kuwa kufanya mapenzi mara nyingi kutakufanya uwe na
furaha zaidi, lakini utafiti mpya umedai kuwa mambo yanaweza kuwa
tofauti.
Watafiti wa Marekani wamebaini kuwa kufanya ngono mara nyingi
kunaweza kupoteza uhalisia, mahaba na hamu. Wanadai kuwa mapenzi ni
‘ubora’ zaidi kuliko ‘wingi’ na kwamba kufanya zaidi kunaweza kuwafanya
wapenzi kuyachoka.
Watafiti kwenye chuo kikuu cha Carnegie Mellon walibaini mwanzo kuwa
ngono na furaha si vitu vya moja kwa moja kama inavyofikiriwa. Kuwa na
furaha kwa mfano kunaweza kumfanya mtu kufanya mapenzi zaidi au kuwa na
afya kunaweza kusababisha mtu kuwa na furaha na kutaka kufanya mapenzi
zaidi.
Kama sehemu ya utafiti huo, wanasayansi waliwafanyia majaribio baadhi
ya wapenzi kufanya mapenzi zaidi. Waliripoti kuwa kufanya mapenzi zaidi
hakukuwafanya wawe na furaha zaidi kwasababu kuongezeka kwa kufanya
kulipunguza hamu na raha ya mapenzi.
Watu 128 waliokuwa na umri wa kati 35-65 waliopo kwenye ndoa (wanawake na wanaume) walishriki utafiti huo.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...