• Home
  • About

Photos: Hiki ndicho alicho enda kufanya Ben Paul Ujerumani...

Kama una mfollow Ben Pol kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii basi  umeshakutana na picha akiwa ughaibuni, yuko nchini Ujerumani na ameeleza kilichompeleka huko.
Ben UJ-2
Ben Pol na Emanuel Austin
Hit Maker wa ‘Sofia’ Ben Pol amesema kuwa ameenda Ujerumani kushiriki katika utengenezwaji wa video ya Mtanzania Emannuel Austin aishiye huko, ambaye alimshirikisha Ben Pol kwenye wimbo wake alipotembelea Tanzania mwaka jana.
Ben UJ-3
Ben Pol akiwa onset na warembo wa Kijerumani
“Kimsingi nipo nchini Ujerumani Frankfurt, niko na mshikaji wangu mmoja anaitwa Emanuel Austin, ni choreographer ni muimbaji ambaye asili yake ni Tanzania lakini yuko based nchini Ujerumani. Mwaka jana alikuwepo Tanzania nilirekodi nae wimbo kwenye studio za Authentic, lakini beat ilifanywa na Fundi Samweli. Kwahivyo sasa hivi tunafanya music video huku Ujerumani tunafanya na the number one producer wa music video huku Ujerumani.” Alisema Ben Pol kupitia 255 ya Clouds Fm.


  Usikilize wimbo wa Emanuel austin akiwa na Ben Paul... Ukiwa na jina Ruka.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...