• Home
  • About

Gari la magereza la shambuliwa kwa ri sasi jijini Dar

  Gari la Magereza lililokuwa limebeba wafungwa na maabusu limeshambuliwa kwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi leo (July 2) katika eneo la Mikocheni, Dar es Salaam.
Akizungumza Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camellius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi.
Kamanda Wambura amesema ni mapema kutaja nia ya watu hao wenye silaha waliovamia gari hilo kwa kuwa wanaweza kuwa na nia tofauti kabisa na fikra za haraka.

Tunafanya uchunguzi ambao utatufikisha mahali tuweze kubaini ni nini. Inawezekana pengine kuna wahalifu walikuwa katika harakati za uhalifu ghafla wakaona basi lile ambalo lina askari wazuri wenye silaha wakaanza kulishambulia…inawezekana. Au inawezekana vingine vyovyote ambavyo hatuwezi kufikiri wala kubaini.” Kamanda Wambura ame sema.
Ameeleza kuwa hakuna maabusu yoyote aliyeweza kutoroka katika tukio hilo na kwamba madhara yaliyotokea kwenye gari hilo sio makubwa. Amesema bado hajapata taarifa yoyote ya uharibifu wa mali au upotevu wa mali uliotokea katika eneo hilo kufuatia tukio hilo.
Akizungumzia watu waliojeruhiwa katika tukio hilo, Kamanda Wambura amewataja watatu waliopata majeraha kuwa ni dereva wa basi hilo, mahabusu mmoja na askari mmoja wa kike.
Kuna baadhi wana michubuko, wale wawili ambao ni dereva na mahabusu mmoja. Lakini kuna askari wa kike ambaye yeye ana majeraha kwenye kifua upande wa kulia. Lakini ni nini kimesababishia michubuko ile hatuwezi kujua kama ni vioo ama ni purukushanai wamejichubua mle ndani au vitu gani.” Amefafanua.
       
                                                         Credit | Timesfm.co

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...