Msanii mkali wa Bongo flavour Linah ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya bila kuachia
wimbo mpya kabla ya kuachia remix ya wimbo wa Kizaizai wa Diamond
ameeleza sababu zinazomfanya aendelee kuishi maisha mazuri hata
anapokuwa hana wimbo mpya redioni kiasi cha kupunguza mfululizo wa
shows.
Linah
amefunguka katika kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio kuwa sababu kubwa
inayomfanya aendelee kung’aa mjini hata bila shows wala kuwa na nyimbo
mpya ni kujipanga mapema kuikabili hali yoyote itakayojitokeza kwenye
maisha yake kama mwanamuziki.
“Labda niseme kitu kimoja, unajua unapokuwa msanii unatakiwa ujipange
vya kutosha. Anything can happen. Kwa hiyo unapofanya kazi at the time
unapokuwa vizuri inabidi ujipange kwa maisha ya mbele pia. Kama mimi
nilikuwa nimejipanga enough kwamba in case ikitokea kitu chochote mimi
niko sawa. Yaani sitatetereka.”
Amesema anajua msanii anapotetereka anamuangusha shabiki wake anapotaka kujigamba kwa wenzake jinsi anavyomkubali msanii huyo.
Credit | Sammisago.com
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...