• Home
  • About

Wa okoaji kwenye meli ya Korea kusini waendelea kuokoa miili ya abiria bila ya kupata mtu hata mmoja hadi sasa..

 
Zoezi la uokoaji katika meli ya Korea Kusini iliyozama linaendelea huku waokoaji wakipata miili ya abiria bila kumpata hata mtu mmoja hadi sasa aliye hai tangu Jumatano ya wiki iliyopita.
Maafisa wa ulinzi wa Pwani ya Korea Kusini wamesema watu 105 wamethibitika kuwa wamefariki na 197 bado hawajapatikana na idadi kubwa ya watu hao ni wanafunzi.

Kwa mujibu wa CNN, waokoaji wameonesha kusikitishwa na hali ilivyo kwa hivi sasa inayosababisha kukosa matumaini ya kupata watu walio hai katika meli hiyo kitu ambacho kinawaogopesha hata kukutana uso kwa uso na familia zinazosubiri majibu kuhusu ndugu zao ambao hawajatoka kwenye meli hiyo.
  “Hali ni mbaya sana, moyo wangu unauma. Tunaenda ndani tukifikiria kwamba huenda tutapata watu walionusurika. Tunapofikia wakati wa kurudi bila kitu, hatuwezi hata kukutana na familia zao uso kwa uso.” Amesema Bard Yoon ambaye ni mmoja kati ya waokoaji.
Kwa upande mwingine, rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amefananisha kitendo kilichofanywa na nahodha wa meli hiyo na baadhi ya wafanyakazi kama mauaji.
“Vitendo vya nahodha na wafanyakazi wengine havikubaliki kabisa, havisameheki na vinaunganishwa kabisa na uuaji.” Amesema rais Park Geun-hye.
Nahodha na wafanyakazi wengine wa meli hiyo tayari wameshakamatwa na kufunguliwa kesi kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...