• Home
  • About

Haya ndiyo aliyo ya sema mugabe juu ya wanao tetea ushoga nchini kwake.


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametishia kuwafukuza kutoka nchini humo wanadiplomasia wanaopigia debe mapenzi ya jinsia moja.Katika hotuba yake ya sherehe za kuadhimisha uhuru wa nchi hiyo, Mugabe alitumia fursa hiyo, kukaripia kile alichokiita upuuzi wa nchi za ulaya zinazohubiri ushogaAlituhumu nchi za ulaya kwa kukosa maadili na kusisitiza kuwa ndoa inaweza kuwa tu kati ya mwanamke na mwanamume.Sio mara ya kwanza Mugabe amekemea swala la ushoga.
Aliwahi kuwataja mashoga kuwa wabaya kuliko Mbwa na Nguruwe.
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Zimbabwe na mashoga hukamatwa mara kwa mara kwa kosa hilo.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...