Makamu mwenyekiti wa bunge maalum la katiba, Samia Suluhu Hassan amesema amepokea hati ya makubaliano ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyothibitishwa kisheria.
Hati
hiyo imefikishwa bungeni hapo baada ya mjumbe wa bunge hilo, Tundu
Lissu kuomba hati hiyo ioneshwe hadharani siku mbili zilizopita.
Waziri
wa nchi ofisi ya rais, Stephen Wasirra alieleza kuwa ametimiza ahadi
yake aliyoitoa awali kuwa hati hiyo ingefikishwa bungeni ndani ya siku
mbili.
Katika hatua nyingine, wajumbe wa bunge hilo maalum la katiba leo wameendelea na majadiliano kuhusu sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya katiba huku suala la muundo wa serikali za muungano likichukua nafasi kubwa.

Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...