• Home
  • About

Kiswahili chatumika kwenye msimu mpya wa tamthilia ya Quantico

Kiswahili kimetumika kwenye episode ya kwanza ya msimu wa pili wa tamthilia ya Quantico ulioanza kuoneshwa Jumapili kupitia runinga ya ABC ya Marekani.

Kinasikika baada ya kundi la watu waliokuwa wamevaa mask kuvamia mkutano ambao Rais wa Marekani alikuwepo pamoja na mke wake. Watu hao wanajiita Citizens’ Liberation Front na wanatumia Kiswahili kuwasiliana.

Msimu wa pili unaendelea kuangalia harakati za kishujaa za wakala wa FBI, Alexandra “Alex” Parrish, nafasi inayochezwa na Priyanka Chopra.
Kwenye msimu wa pili yumo staa wa Afrika Kusini, Pearl Thusi anayetumia jina Dayana Mampasi kwenye tamthilia hiyo.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...