• Home
  • About

Dogo janja : Sija wahi ku andikiwa nyimbo na Darasa...

Rappper kutoka TipTop Connection,Dogo Janja amekanusha kuandikiwa nyimbo na rapper Darasa.Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Darasa kudai kuwa anajuta kumuandikia Janjaro track inayofahamika kama “Ya Moyoni”,kwani licha ya kutolipwa,ilimsababishia lawama kati yake na baadhi ya watu.
“Sijawahi kuandikiwa nyimbo na Darasa,wala hatukuwahi kuwa na makubaliano yeyote ya yeye kuniandikia nyimbo,tulikua studio pamoja ni kama alikua akinipa idea tu lakini ngoma niliandika mwenyewe”aliongeza Janjaro.
                                                                   
Kuhusu tetesi za kutokua na maelewano mazuri na Paka rapper  Young Dee,rapper huyo anaefanya vizuri na ngoma yake ya “My Life”,amedai hana ugomvi na Young Dee kama baadhi ya watu wanavyodhani na hategemei kuwa na ugomvi na msanii yeyote.Teamtz.com ilipomuuliza kama  yupo tayari endapo ikitokea Young Dee anataka kufanya collbo na yeye,Janjaro alijibu “mpaka sasa nina collbo mbili tu,na kama ikitokea nafanya collabo ntafanya collabo na wasanii wenye future,sio tu kufanya collabo,nafikiria kufanya collbo na mtu mwenye mipango”Janjaro alijibu.

Credit:teentz

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...