• Home
  • About

Jay Z a ondoa albamu zake zilizo baki kwenye mtandao wa Spotify...

   Ni kitu ama jambo la ajabu iwapo utakubali kuacha album zako kwenye mtandao wa mpinzani wako mkubwa, ndicho alichokifanya Mmiliki wa mtandao wa Tidal, Jay Z.
Muda mfupi baada ya kuzindua Tidal mwaka jana, Jay Z aliiondoa album yake ya Reasonable doubt kwenye mtandao wa Spotify , lakini wiki iliyopita rapper huyo amemalizia na album zake zote za mtililiko wa Blueprint.

Japo baadhi ya nyimbo zake bado zinapatikana kwenye mtandao huo, lakini Album zake hizo kubwa  kwasasa zinapatikana exclusively kwenye mtandao wa Tidal tu.
Hii imekuja siku chache baada ya tetesi za kuwa mtandao wa Spotify ulikua umepanga kujiunga na Tidal.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...