• Home
  • About

Dr.Mohamed Shein atangazwa kua raisi wa Zanzibar , Ashinda kwa asilimia 91.4


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha amemtangaza Dr. Mohammed Shein kuwa Rais wa Zanzibar kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016 kwa asilimia 91.4.


Kwa mujibu wa Jecha, Shein amepata ushindi wa kishindo wa kura 299,982 ambazo ni sawa na asilimia 91.4. Nafasi ya pili imeshikiliwa na mgombea urais wa ADC, Hamad Rashid aliyepata kura 6,734 huku Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 6,076.
Kutokana na matokeo hayo, Dk. Ali Mohamed Shein ndiye atakayeendelea kuiongoza Zanzibar kwa muhula wake wa mwisho kwa mujibu wa Katiba.
Hatua hiyo imekuja baada ya kujitokeza dosari katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka jana na kuamriwa uchaguzi huo kurudiwa.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...