• Home
  • About

Hii ndio filamu ya kibongo ilio malizika muda mchache tuu baada ya kutoka.

Nakala za filamu mpya ya JB na Wema Sepetu, ‘Chungu Cha Tatu’ zilizoingia sokoni Jumatatu hii zimemalizika ikiwa ni siku tatu toka iachiwe.

JB alisema kasi ya mauzo ya filamu hiyo, ina kila dalili ya kuvunja rekodi ya filamu yake iliyopita Mzee wa Swagga.
“Filamu inaenda vizuri sana, Jumatatu baada ya kuingia sokoni masaa manne kopi zilizoingia sokoni ziliisha, Jumanne tukazalisha tena zikaisha, leo hii tumezalisha nyingine nyingi kwa sababu hata mikoani nilipigiwa simu kwamba zimeisha. Kwahiyo nashukuru mashabiki kwa kuonesha kuniunga mkono,” alisema JB.
JB alisema filamu hiyo imemgharimu takriban shilingi milioni 68 mpaka kukamilika.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...