Siku kadhaa zilizopita mtayarishaji wa muziki wa studio ya The
Industry, Nahreel alilalamikia kitendo cha utambulisho wake ‘Nahreel on
the beat’ kuondolewa kwenye hit song ya Diamond Platnumz ‘Nana’ ambayo
ndiye aliyei-produce.
Diamond naye amepata nafasi ya kueleza sababu ya utambulisho huo kutokuwepo kwenye wimbo huo.
Baba Tiffah amesema kuwa mwanzoni wakati anataka kushoot video hiyo
Nahreel alimpa demo ambayo ilikuwa bado haijawekewa sign hiyo, hivyo
baada ya kushoot na director kumaliza ku edit, alipopewa audio ambayo
imekamilika ikawa imeongezwa sign, kitu ambacho kwa director ingempa
kazi kutokana na kuongezeka kwa sekunde ambazo kwenye demo iliyotumika
mwanzo hazikuwepo.
“so mara ya pili alivyonipa sasa video ilishaisha nataka iliyokuwa
mastered akawa ndio ameweka sign” amesema Diamond kupitia 255 ya XXL.
“Haikuweza kufit kwasababu ilikuwa inazidisha sekunde halafu ilikuwa
inaanza mwanzo mara kumi ingekuwa mwisho…inamaana editor aanze
kukatakata na kuedit tena upya kitua ambacho tulikuwa tumeshachelewa.
Kwahiyo ilichelewa kuwekwa ingekuwa imewekwa kuanzia mwanzo ingekuwa
rahisi lakini sina sababu ya kusema nimkate producer kwasababu kama
producer kafanya kazi yake kubwa lazima apewe credit zake.” Alisema
Diamond.
“Ile nyimbo imefanyiwa mastering na Tudd Thomas, mtu anaweza kusema
labda Tudd Thomas ndo kaichekecha, sio kweli ilichelewa na sioni sababu
ya kumfanya Mtanzania mwenzangu kutokumpa credit zake katika nyimbo
aliyoitengeneza katumia jasho lake nitakuwa na roho mbaya sana. Director
akasema nataka iwe kama ilivyokuwa mwanzo mkinipa nyingine haiwezi
kufit, aah sasa ntafanyaje kitaalam mi sijui nikaona basi tukachukua ile
ile ya mwanzo.” Alimaliza Diamond.
source 255 ya XXL clouds.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...