• Home
  • About

Producer sheddy clever atoa sababu za kwanini wasanii wa hiphop hawa record kwake..

     Producer wa Burn Records aliyetengeneza hits kadhaa za wasanii wa kuimba kama Diamond na wengineo , Sheddy Clever aki ongea kwenye Planet Bongo ya East africa Radio amesema kuwa anatamani pia kufanya kazi na wasanii wa Hip Hop na kutaja sababu za kwanini wasanii wengi wa Hip Hop hawaendi kurecord kwake.
Sheddy amesema kuwa sababu kubwa inayowafanya wasanii wengi wa Hip Hop kutomfata kufanya naye kazi ni kutokana na kuwa wanamskia akitengeneza zaidi kazi za wasanii wa kuimba.

  Amewataja wasanii wa Hip Hop ambao anatamani kufanya nao kazi kuwa ni Joh Makini na Fid Q.
“Natamani sana kufanya kazi na msanii kama Joh Makini, Fid Q” alisema Sheddy
  “Lakini unajua inakuwa ngumu kwasababu gani unajua, wanaona tutaenda vipi kwa Sheddy jamani kila siku tunasikia tu ngoma ngoma za kuimba wabana pua, kwahiyo wanakuwa wanakosa ule moyo.”

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...