• Home
  • About

Hiki ndicho hackers walicho mfanyia Director Nisher

Akaunti ya Instagram ya Director wa Music video, Nisher baybe imefungwa baada ya kuwa ‘hacked’ na watu wasiojulikana.

Baada ya watu hao wanaojiita fakewatchbusta kuhack akaunti yake walipost picha yake akiwa amevaa saa za thamani na kuweka maandishi yenye rangi nyekundu FAKE!
nisher
“Kuna watu wamenitag kwa jamaa wa saa feki (fakewatchbusta ) jana so hao jamaa waliponipost kwao wakahamia kwenye page yangu nakuanza kutuma spam messages na comments mwishowe waka hack account,” Nisher alisema.
“Hiyo account ya saa feki ukiichunguza wanawafutilia maceleb wakubwa. Wameshamfuatilia Floyd Mayweather, Rick Ross, Soulja Boy, Dj Mustard na wengine kibao so sishangai kabisa,” ameongeza.
20150611051001
“Wakaanza kubadilisha usernames na kupost picha chafu so mi nilichofanya ikabidi nitoe report Instagram kuwa nimekuwa hacked wakaifunga.”
Hata hivyo Nisher amesema saa zake zote ni halisi.
“Zote ni real,” amesema Nisher.
“Japo kwa mara nyingine imebidi nimpigie agent wangu nimuulize kuwa inakuaje naambiwa hii saa ni feki! Yeye mwenyewe ameshangaa sana so anacheki na duka aliponunulia huko UK,” ameongeza.
“Kitaeleweka tu. Japo sishangai chochote maana kama wameweza kumwita Rick Ross na Floyd Mayweather FAKE na wao ni Multi-Millionaires, sembuse mimi wakuzikusanya kwa msimu.”
20150611044235
Saa halisi za Nisher zikiwa kwenye boksi yake
Kuhusu bei ya saa zake hizo, Nisher amesema kuwa hawezi kuitaja kwa sababu za kiusalama.
“Siwezi kutaja hewani but receipts zipo so kama mtu anataka kujua how much I bought it karibu home, It’s crazy! Nashindwa kutaja kwasababu ya security reasons, sio kwaajili ya hofu.”
Hata hivyo Nisher anahisi kuna watu wengi wanaomchukia hasa wanaume wenzake.
“Nimejifunza kuwa naonewa wivu sana na wanaume wenzangu,” amesema muongozaji huyo. Sijui kwanini, sababu aliyenitag kwenye hiyo site ni mtangazaji wa radio na TV, simtaji jina cuz he’s not even worth it! Ila team yangu imeshamfuma na alipoona account yangu inashambuliwa aliwatag wenzake na kuwaambia “we did it!!” So message kwake nampa pole kwa kusosa kazi za kufanya.”
credit: bongo5

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...