• Home
  • About

Dogo janja 'Sina ngoma mpya lakini kila siku na kwea pipa kupiga show mikoani'

 Dogo Janja hana ngoma yoyote mpya lakini kila siku amekuwa akikwea pipa kupiga show mikoani – thanks kwa mashavu wanayopata wasanii wa Tip Top Connection.

Dogo Janja (kulia) akiwa na Madee
Dogo Janja ameiambia Bongo5 kuwa licha ya kuwa hajatoa ngoma yoyote ndani ya kundi hilo lakini anaishi maisha mazuri.
“Nashukuru Mungu nipo mikono salama, naishi vizuri Tip Top ingawa sijatoa ngoma mpaka sasa. Naishi vizuri yaani maisha ni mazuri tu,” amesema Janjaro.
“Unajua ndani ya Tip Top kuna utaratibu wa kutoa ngoma kwa zamu, hivi karibuni itasikika ngoma ya Raymond, halafu itakuja ya Tip Top na baada ya hapo utasikia yangu. Kwahiyo mimi nasikilizia utaratibu.”

credit: bongo5.com

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...