Kwa siku ya jana tarehe 7 mmoja kati ya wa kongwe ama kiongozi wa Yamoto band Aslay Isihaka alikua aki sherehekea siku yake ya kuzaliwa huku watu wengi waki mtaki heri na pongezi, MMoja kati ya watu hao ni Meneja wa kundi hilo Said Fella. Said fella ali weza ku mpa Aslay zawadi ya gari kwa siku yana, Gari hilo likiwa ni jipya..
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Fella alipost picha alipokuwa akimkabishi gari hiyo na kuandika ujumbe mrefu wa kumpongeza.
“MUNGU
NDIO KILA KITU TATIZO MUDA NA SUBRA INSHAALLAH MWANETU ASLAY KITUO
CHETU CHA MKUBWA NA WANAWE YOUTH CENTRE TEMEKE MIKOROSHINI TUNAJUA
MCHANGO WAKO TANGU TUANZISHE KITUO IKI LEO TUMEONA WACHA TUKUZAWADIE
NYEZO ILI MURADI IWE CHANGAMOTO KWA WENZAKO KITUONI APA KUONGEZA BIDII
NA UPENDO NA KUJITOA KUSAIDIA WENZAO KAMA ULIVYO JITOA WEWE KWA WENZAKO
INSHAALLAH MUNGU TUBARIKI SOTE SIE NA WADAU WETU PIA ATULINDIE AMANI
YETU.baadaye tukutane matei jijini dodoma kwa burudani ya mkubwa na
wanawe ya moto band njoo tucheze ngoma ya vijana mpya kimadoido.”
Aslay naye alipost picha hiyo na ujumbe mrefu wa shukrani.
“Asante mungu Kwa kunipa uhai Na kipaji ambacho leo hii kina fanya
naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono Ya mtu mwenye
moyo wa kibinaadamu. Najua kuna mengi makubwa ambayo boss wangu
@mkubwafella umenifanyia ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati
wake haujafikia ila naomba nichukue fulsa hii kukushukuru kwa hiki
ulichonifanyia leo katika sherehe Ya kusherehekea siku yangu Ya kuzaliwa
umenifanya nijione mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo
itakuwa siku yangu ya kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata Nije kuwa
bilionea @mkubwafella asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama
mimi sikuiwazia kabisa kama Leo nitapata gari Na ninaushukuru uwongozi
mziki Wa #mkubwanawanawe pamoja na manager wangu @chambusso boss wangu
@babutale @mhtemba na mama yangu @sweatfella bila kuwasahau wasanii
wenzangu wa @yamoto_band mungu ndie atakaewalipa … Nawatakia usiku mwema
woote na Watu wa Dodoma Tukutane kesho pale Matei.”
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...