Rais wa Marekani Barack Hussein Obama, ameendelea kuonyesha mapenzi
na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, ambacho siku mbili zilizopita
kilishindwa kufanikisha safari ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali
ya michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazil.
Obama, ameonyesha kuwa pamoja na wachezaji wa The Yanks, baada ya
kupiga simu kwenye kambi ya timu ya taifa ya Marekani na kuzungumza na
nahodha Clint Dempsey pamoja na Tim Howard, ambapo amesikika
akiwapopngeza kwa niaba ya wachezaji wenzao.
Obama, hakusita kumpa shukurani mlinda mlango Tim Haward kwa kazi
nzuri aliyoifanya wakati wote wa michuano ya kombe la dunia ambapo
alionekana kuwa kisiki kwa timu pinzani pale walipolishambulia lango la
USA.
Hata hivyo raisi huyo wa Marekani amemtaka mlinda mlango huyo wa
klabu ya Everton ya nchini Uingereza, kujitayarisha na mapokezi makubwa
kutoka kwa mashabiki wa soka nchini humo, kufuatai kazio nzuri
aliyoifanya.
Katika kufikisha salamu hizo Obama amemkebehi Howard, kwa kumwambia
kutokana na maandalizi yanayofanywa na mashabiki huko nchini Marekani,
hana budi kukata ndevu ili kupunguza usumbufu, ambao utapoteza kumbu
kumbu kwa walio wengi kuitokana na shauku waliyonayo dhidi yake.
Katika hatua nyingine Obama amewaambia wachezaji wa timu ya taifa ya
Marekani ni vipi alivyoumizwa na hatua ya kutolewa kwenye fainali za
kombe al dunia za mwaka huu, lakini akawasisitiza kutokuwa na hofu
yoyote kwani mpango mkakati wa nchi hiyo kwa sasa ni kutaka kuona soka
linachezwa kuanzia ngazi ya vijana wenye umri mdogo.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...