• Home
  • About

Adam juma ku fanya kazi mbili kubwa na Prof.J pamoja na Roma, aandika kua ana ipenda kazi yake kuliko wanavyo dhani..

 Ngoma ya kipi sijasikia ni wimbo mkubwa wa msanii mwenye heshima kubwa katika game la bongo flava na asiyechuja, Profesa Jay ambaye amemshirikisha msanii anae-kick zaidi katika kizazi cha bongo flava kinachoanza miaka ya 2000, Diamond Platinumz.
Lakini pia moja kati ya nyimbo zilizokuwa na utata na kuvuta usikivu wa watu wengi ni wimbo wa KKK(Karibu Kwenye Karamu) wa Roma Mkatoliki ambaye siku zote akitoa wimbo huzua  mada nyingi kwenye media na mitandaoni huku akizungumzia mambo mengi katika dakika chache za wimbo wake.
Profesa Jay na Roma Mkatoliki wote wame zungumzia  video zao zinazofanyika hivi karibuni ambapo wote wamemtaja muongozaji mkongwe wa video za muziki Tanzania, Adam Juma kuwa ndiye atakayeongoza video hizo.
“Video ataisimamia director anaitwa Adamu Juma wa Visual Lab. Watu wanamjua ndiye director bora zaidi wa video aliyewahi kutokea Tanzania na ameboresha sana mashine zake, ameboresha sana vitu vingi.” Amesema Profesa Jay.
Katika video hiyo itakayofanyika Jumamosi, July 12  Profesa Jay amewaalika mashabiki wote kuvaa smart kwa jinsi wanavyoweza na kushiriki kwenye video hiyo.
Kwa upande wa Roma ame sema kuwa atafanya video yake na Adam Juma na kwamba wataifanya katika mazingira tofauti ambapo vipande vingine vitashutiwa mikoani.

Katika hatua nyingine, Adam Juma ameandika kwenye Instagram ujumbe unaoleza kuwa anaipenda sana kazi yake ya kuongoza video za muziki na kwamba anaipenda kwa sababu imemkutanisha na watu wengi.
 "Wengi wana fikiri kila kitu ni ushindani, sio kweli. Ilove this job, Ithink naipenda hii kazi kuliko watu wanavyo chukulia , naipenda kwa sababu imeni kutanisha na watu wengi ambao wame badilisha maisha yangu  na nawashukuru sana katika muda wangu wa miaka kumi nime ona mengi mazuri na mabaya ila mazuri mengi. Wapo nilio wa kosea naomba muni samehe mimi bina adamu na kuna wale nime wasaidia sana naomba muwasaidie na wengine, Kwa wano nijiua mimi sio mchoyo wa kufundisha  kama mtu ana taka kujifunza kweli. Cinematography is an art . Ilove this art"

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...