Mara nyingi tumezoea kuona wasanii wa Tanzania wakiomba kufanya
collabo na wasanii wakubwa wa kimataifa kwa lengo la kujitangaza
kimataifa, lakini Diamond Platnumz amefikia hadhi ya yeye kuombwa
collabo na wasanii wakubwa kama Mafikizolo kutokea South-Africa.
Kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini limemuomba hit maker wa ‘Number 1′
Diamond Platnumz afanye nao collabo, na jana (June 9) waliingia katika
studio ya Oskido iliyoko Johannesburg kurekodi wimbo huo.
“We doing a collaboration with Diamond,the song is sounding awesome yes”
aliandika Theo Kgosinkwe wa Mafikizolo katika moja ya picha wakiwa
studio na Diamond.
Kupitia Collabo hiyo ya Mafikizolo na Diamond itampa nafasi nzuri zaidi
Platnumz sababu ya ukubwa walionao wanamuziki hao wa Afrika Kusini.
Mafikizolo ni washindi wa Tuzo mbili za MTV (MAMA) 2014 zilizofanyika Jumamosi iliyopita huko Durban, Afrika Kusini.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...