Akiwa mmoja wa
waandishi maarufu zaidi kwa miaka 50, Angelou anajulikana zaidi kwa
kitabu chake cha mwaka 1969, I Know Why the Caged Bird Sings. Kilikuwa
ni kitabu cha kwanza kati ya saba ya vitabu kuhusu maisha yake kuanzia
mateso aliyopata miaka ya 1930s.
Hapa akipewa Pongezi na rasi Barack Obama
I Know Why the
Caged Bird Sings, kilichoandika kuhusu ubaguzi wa rangi na mateso ya
familia wakati akikua kilikaa miaka miwili kwenye orodha ya vitabu
vilivyouza zaidi. Vitabu vyake vingine ni pamoja na Just Give Me a Cool
Drink of Water ‘fore I Diiie (1971), And Still I Rise (1978), Now Sheba
Sings the Song (1987), na I Shall Not Be Moved (1990).
Vitabu alivyowahi kuviandika katika picha'kulia'
Shairi lake ‘On
the Pulse of the Morning’ lililoandikwa kwaajili ya sherehe ya
kuapishwa kwa Rais Bill Clinton liliwagusa wengi na kuuza kopi zaidi ya
milioni moja Marekani. Alipewa pia kazi ya kuandika mashairi kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Mataifa mwaka 1995 na alimkumbuka Nelson Mandela
kwenye shairi kwaajili ya ikulu la Marekani mwaka jana.
Angelou pia aliongoza filamu Down in the Delta, iliyoshinda tuzo tatu za Grammy kwa album ya maneno ya kuongea.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...