• Home
  • About

Huyu ndiye alie andika wimbo wa 'Happy' Ulio imbwa na Phareell Willium

  Baada ya kupita wiki kadhaa ya rekodi kuvunjwa na single yake ya ‘happy’ mwimbaji Pharrell Williams kwenye show ya Howard Stern ameeleza wazi kwamba single hiyo sio yake bali ni wimbo ambao uliandikwa na Cee-Lo Green na hakua anafahamu kuhusu wimbo huo mpaka pale Green alipoamua kumpa na kumruhusu aimbe.

 Hii ni mara ya pili Williams anapata kitu kutoka kwa Cee-Lo sababu pia amechukua nafasi yake kama kocha mpya wa season ya saba kwenye mashindano ya kuimba ya The Voice.
Cee lo Green staa wa hit ya 'forget you'
                                  Cee lo Green
Kabla ya noma yake  “Happy” phareel alikua ni Producer na mwimbaji ambae amewahi kuingia kwenye headlines za chati za muziki duniani kwa single kama kolabo na Snoop Dog na Jay Z na amewahi kuwaandikia nyimbo wakali kama Kanye West, Gwen Stefani, Gloria Estefan.
Pharrell pia aliwahi kumuandikia Michael Jackson enzi hizo lakini wawili hao hawakuweza kufanya kazi pamoja na nyimbo nyingi ziliishia kutumiwa na Justin Timberlake kwenye Album yake ya 2002 Justified.
Pamoja na kwamba Pharrell alimuandikia Michael Jackson hizo nyimbo hizo anasema timu yake ilizikataa, yani timu ya MJ ilizikataa hata baada ya Michael Jackson kuzipenda na kuzikubali nyimbo hizo baadae.
‘Nimefanya nyimbo nane kwa ajili ya Michael lakini zote hazikumfikia na ziliishia kurekodiwa na Justin Timberlake lakini baadae Michael mwenyewe aliniimbia hizo nyimbo na kusema zilitakiwa ziwe zake na nikamjibu kuwa zilikua za kwako’
 CREDIT | Millardayo.com

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...