Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa
Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4
ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku
Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa
asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi
huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate
kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .
Kesi Mahakamani
Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu
mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa
kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye
utata.
Na kwamba sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.
Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote
lakini siku moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na
mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na
Blantyre.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...