• Home
  • About

Beyonce yu mjamzito tena...

  Wasanii wawili wakali wa Marekani Jay Z na Beyonce wameripotiwa kuwa wanatarajia kumpata mtoto wao wa pili na kwamba wao wameifanya iwe siri.
Tetesi za ujauzito wa Beyonce zimeelezwa na Jarida la OK! Kuwa wawili hao walikuwa na mpango wa kumpata mtoto wa pili tangu February.

“Marafiki zake tayari wameshawishika kukubali kuwa ana ujauzito, vitu anavyomtokea vinafanana na vile alivyokuwa na uja uzito wa Blue Ivy.” Chanzo kimeliambia jarida hilo.
Nao mtandao maarufu wa udaku, MediaTakeOut umeripoti kuwa mfanyakazi wa Barclays Center ameueleza kuwa Beyonce huwa siku zote anakunywa Vodka anapokuwa katika eneo hilo lakini siku hizi amebadilika na anakunywa vinywaji laini na maji.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa kimemuona Beyonce mara kadhaa akitumia vidonge vya vinavyotumiwa na wajawazito ‘organic folic acid pills’.
Wakati tetesi hizo zikiendelea Beyonce na Jay Z wamepanga kufanya ziara ya pamoja katika majira ya joto na watapiga show kwenye viwanja 20 tofauti.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...