• Home
  • About

VIDEO | Drake ajibadili kwaku vaa wigi naku ingia mtaani kuhoji watu juu ya wanavyo mchukulia...

  Inahitaji moyo wa ziada kuingia mtaani na kuwahoji watu wewe mwenyewe kuhusu ‘wewe’ na kisha kupata baadhi ya maoni hasi na yanayokuponda moja kwa moja kutoka kwa watu wanaodhani wanaongea na mtu mwingine.

Rapper toka Canada, Drake alikuwa sehemu ya show ya ‘Jimmy Kimmel Live’ ambapo alivaa wigi lenye ndevu za bandia ili kuficha sura yake asitambulike, na kisha kama mwandishi wa habari mcheshi akakusanya maoni ya watu katika mitaa ya Hollywood ikiwa ni sehemu ya segment ya I witness News.
Drake alikuwa anawauliza watu hao mtazamo wake kuhusu ‘Drake’ alivyohost katika tuzo za ESPY ambazo hata hivyo hazijafanyika bado.
Moja kati ya mashabiki wake ambaye hata kama hajawahi kuona maoni yake yalikuwa mazuri tu kuwa ‘aliua mbaya kwenye show hiyo’, “Drake definitely killed it’.
Lakini mwanamme mwingine alipoulizwa yeye alitoa makavu live kuwa hampendi Drake na anadhani ni muigizaji na wala sio rapper.
“I don’t like Drake, I think he’s an actor, he’s not a real rapper.” Alisema.
Wapo waliosema hawampendi na wengine wakasema sio mashabiki wake kabisa. Lakini yote aliyameza na kuendelea kuhoji tena kwa ucheshi wa hali ya juu.
Hata hivyo, alipojaribu kuwauliza itakuwaje kama akiwaambia kuwa wanaengea nae ni Drake, wengi walikuwa hawaelewi.
“I would say I’m idiot, totally idiot.”
Kijana mmoja yeye aliambiwa arap wimbo mmoja wa Drake na mwisho alikuwa surprised pale Drake alipotoa wig na ndevu za bandia na kuonesha kuwa ni yeye kweli.
Shabiki huyo alialikwa kwenye show ya Jimmy Kimmel Live akiwa na Drake.


Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...