• Home
  • About

Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya kikwete asema ni ukosefu wa adabu kuwa tukana wa asisi wa Tanzania.

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete  akizungumza na Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari usiku wa juzi, Jumatano, Aprili 16 katika mahojiano maalum ya kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano, Rais Kikwete amesema: kuwa ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu, kwa baadhi ya Wa Tanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli Waanzilishi wa Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume.


Rais Kikwete amesema kuwa viongozi hao wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi makubwa na ya kihistoria, kiasi cha kwamba Watanzania wanao wajibu wa kudumisha na kuenzi heshima yao kwa namna ya kudumu.

Rais Kikwete ametoa msimamo huo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu matusi, kejeli, dhihaki ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache wa Bunge Maalum la Katiba juu ya waasisi hao wa Tanzania na Wabunifu Wakuu wa Muungano wa Tanzania.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...