Majaji wa Shindano la
Kusaka la Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie
Talents wakijadiliana jambo wakati wa Zoezi la kusaka vipaji vya
uigizaji kuingia Hatua ya pili kwa washiriki waliofanikiwa kupita kwenye
mchujo.Kulia ni Single Mtambalike (Rich Rich), Ivon Chery (Monalisa) na
Roy Sarungi.
Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili wakifanyiwa usaili kwa ajili ya hatua ya pili sasa.
Muongozaji wa Mradi wa
Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama
Tanzania Movie Talents, Bw Stanford Kihole (kulia) akitoa maelekezo kwa
washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili katika mashindano ya
kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania likiwa limeaingia hatua ya pili
Mkoani Mwanza.
Baadhi ya Washiriki
waliofanikiwa Kuingia katika Hatua ya Pili ya Shindano la Kusaka Vipaji
vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa
makini kusikiliza maelekezo juu ya hatua ya pili waliofanikiwa kuingia.
Baadhi ya washiriki
waliofanikiwa kuingia hatua ya pili wakiwa mbele ya majaji kwaajili ya
kupewa maelekezo ambapo washiriki watapewa muswada (script) kwaajili ya
hatua ya pili ambapo wataingia wawili wawili na kuanza kuonyesha vipaji
vyao.
Kikosi Kazi kikiendelea
kurekodi matukio yanayoendelea katika Shindano la Kusaka Vipaji Vya
Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents linaloendelea
kufanyika Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza.
Baadhi ya washiriki
waliofanikiwa kuingia hatua ya pili katika Mashindano ya Kusaka Vipaji
vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa
makini katika kupitia muswada (script) waliopewa na majaji ili waweze
kusoma na baadae kuingia mbele ya majaji na kuonyesha vipaji vyao
kutokana na muswada (script) waliopewa.
Baadhi ya washiriki
waliofanikiwa kuingia hatua ya pili wakifanya mazoezi mara baada ya
kupewa muswada (script) na majaji kabla ya kwenda kuonyesha vipaji vyao
mbele ya majaji.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...