Watafiti nchini Uingereza wanasema kula matunda na
mboga za majani mara saba kwa siku inakuwezesha kuwa na afya zaidi
kuliko mara tano iliyokuwa imependekezwa hapo awali na shirika la afya
duniani
Utafiti huu mpya unasema kuwa kula matunda mara saba kwa siku kunaweza kuokoa maisha yako kutokana na vifo vya mapema.
Wataalamu wanasema kuwa mifumo mingine ya maisha
kama vile kutovuta sigara na kutokunywa pombe kupindukia pia imechangia
kupungua kwa vifo.
Wanasema kuwa hawakuzingatia tu faida za Matunda na mboga bali mambo mengine mengi.
Watafiti katika Chuo kikuu cha University
College London, walitathmini Data iliyokusanywa kati ya mwaka 2001 na
2008, iliyowapa mweleko kuhusu afya ya watu wanaokula matunda kwa wingi.
Utafiti huo ulitathmini idadi ya vifo kwa ujumla pamoja na vifo vinavyotokana na Saratani, maradhi ya Moyo na Kiharusi na kugundua kuwa vifo vya mapema vilipungua kulingana na mtu anavyokula matunda na mboga za majani.
Mboga za majani ndizo zilikuwa na uwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi hjata zaidi ya matunda.
Maji ya matunda hayakuwa na manufaa makubwa huku matunda yanayopakiwa kwenye mikebe yakionekana kuongeza tisho la kifo.
Wataalamu wanasema kuwa wangali wanaendelea na utafiti wao na kwamba kuna mambo mengine mengi yanayochangia afya ya mtu.
-BBC
Wanasema kuwa hawakuzingatia tu faida za Matunda na mboga bali mambo mengine mengi.
Utafiti huo ulitathmini idadi ya vifo kwa ujumla pamoja na vifo vinavyotokana na Saratani, maradhi ya Moyo na Kiharusi na kugundua kuwa vifo vya mapema vilipungua kulingana na mtu anavyokula matunda na mboga za majani.
Mboga za majani ndizo zilikuwa na uwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi hjata zaidi ya matunda.
Maji ya matunda hayakuwa na manufaa makubwa huku matunda yanayopakiwa kwenye mikebe yakionekana kuongeza tisho la kifo.
Wataalamu wanasema kuwa wangali wanaendelea na utafiti wao na kwamba kuna mambo mengine mengi yanayochangia afya ya mtu.
-BBC
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...