Klabu ya Azam FC imeanza rasmi maandalizi ya kutetea ubingwa wao
msimu ujao na michuano ya kimataifa kwa kukamilisha usajili wa mchezaji
wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Yanga.
Taarifa rasmi zilizothibitishwa na meneja wa Azam FC Jemedari Said ni
kwamba mshambuliaji Didier Kavumbagu amejiunga na klabu hiyo kwa
mkataba wa mwaka mmoja.
“Ni kweli Kavumbagu tumemalizana nae na amesaini mkataba wa mwaka mmoja. Taarifa zaidi zitatolewa baadae.” Alikaririwa Jemedari.
Kavumbagu alitua nchini Tanzania akitokea Burundi alipokuwa
anaitumikia Vital O na kuja kujiunga na Yanga misimu miwili iliyopita.
Credit /millardayo.com
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...