• Home
  • About

Vcto valdess hatihati kukosa fainali za kombe la dunia mwaka huu Brazill.

Mlinda mlango wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona Victor Valdes, huenda akazikosa fainali za kombe la dunia za mwaka huu 2014, kutokana na jeraha la goti alilolipata wakati wa mchezo wa La Liga, uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Celta Vigo.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, alipatwa na maumivu ya goti la mguu wake wa kulia, baada ya kufanikiwa kudaka mpira wa adhabu ndogo katika dakika ya 23, ya mchezo huo ambao ulichezwa Camp Nou.
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Barcelona imeeleza kwamba tayari Valdes ameshafanyiwa vipimo na imabainika tatizo linalomkabili linahitaji upasuaji, hali ambayo huenda ikamuweka nje kwa zaidi ya miezi miwili.
Victor Valdes, alikua anafikiriwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, kutokana na kiwango kizuri alichokionyesha tangu mwanzoni mwa msimu huu, huku baadhi ya wadau wa soka nchini humo walidhania huenda angempiku mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa ya nchi hiyo Iker Casillas.

Endapo Victor Valdes, atashindwa kwenda nchini Brazil katika fainali za kombe la dunia nafasi yake itachukuliwa na mlinda mlango Diego López ambae ni chaguo la kwanza la meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Anceloti.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...