Diamond Platnumz amesema katika label yake ya WCB, yeye
huchangia vitu vidogo sana na kwamba management yake chini ya Babutale
na Mkubwa Fella ndiyo wanaowaangalia wasanii na kuona kama wasanii hao
wana vipaji na uvumilivu.
Akiongea na East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo, Diamond Platnumz alisema:
“Kiukweli wasanii wanaokuja kwenye label yangu mimi huwa si mchunguzi
sana, lakini management yangu ndiyo huwa inaangalia wakina bosi Tale na
Mkubwa Fella wao ndiyo wanaangalia huyu msanii ana kipaji au hana. Wao
ndiyo wanajua huyu mambo iko huku au hamna. Wao wanaangalia vitu vingi
wanaangalia kama msanii ni mvumilivu. Hivyo kuna vitu vingi wao wanakuwa
wanaangalia kutokana na uzoefu wao katika muziki na kudeal na wasanii.
Kuna wasanii wanaweza kula msoto mpaka unawaonea huruma, lakini ndiyo
hivyo ukitaka kuingilia tu watakuwambia ‘hapana usiingilie tuache kuna
jambo tunalitazama.”
Staa huyo aliongeza na kusema yeye mchango wake huwa ni mdogo kwa
mfano katika hatua za mwisho kuona msanii yupi anastahili kutoka kwa
wakati upi, au kama msanii ana mapungufu fulani yeye anaweza kuchangia
mawazo labda msanii huyo afanye kitu gani ili mwisho wa siku aweze
kutoka.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...