Mmmoja wa mapacha wa wili walio kua waki unda kundi la P-squre Paul ame amua kuji shusha naku muomba msamaha kaka yake Putter .
Pacha huyo wa kundi la P-Square lililovunjika ameandika maelezo marefu kwenye Instagram kuelezea hali halisi ilivyo:
Mnachotaka ni P-Square, ninachotaka ni familia, upendo na kujali.
Mitandao ya kijamii ni mzizi mpya wa maovu. Kuna familia kabla ya
Psquare na siku zote kutakuwepo familia baada PSquare. Jude alikuwa
chambo na mhanga tu. Mtu ambaye amekuwa akituweka pamoja kwa miaka yote
hii. Ukweli ni kwamba Peter na Paul wana matatizo.
Kwa mara ya kwanza nimeamua kufanya kitu nje ya Psquare, na huo ndio
mfano hapa. Nimekuwa nikimuunga mkono kaka yangu kwa asilimia 100
kuanzia kwenye endorsement zake peke yake hadi kwenye Dance with Peter
ambazo zingine bado zipo kwenye Instagram yangu.
Na sasa nina maswali matatu:
1.Kwanini haya mambo yanatokea muda mfupi baada ya kutoa single ya Muno chini ya Rudeboy Records?
2. Ni vipi baada ya Jude kuacha kuisimamia Psquare kwa zaidi ya mwezi sasa, matatizo bado yanaendelea?
3. Kwanini (Peter) ana haraka hivyo ya kuwa msanii anayejitegemea?
Inahuzunisha sana, na inavunja moyo sana, natamani mambo haya
yasingefahamika hadharani. Na sasa mashabiki wetu wamegawanyika,
tafadhali msiunge mkono ujinga wa teamPaul sihitaji hayo. Tafadhali
mjizuie sababu ni uovu. Na kwa mapromota, kumuunga mkono Peter
akitumbuiza nyimbo za PSquare peke yake jukwaani, mnatuua na kutuharibu
sisi zaidi.
Mpendwa kaka yangU nakuomba, hata kama humtaki tena Jude na hauitaki
psquare, milele utakuwa kaka yangu. Lakini natamani sisi watatu
tungeendelea kuwa pamoja sababu ni kitu cha furaha. Watu wanatupenda
sana si sababu tu ya muziki wetu mzuri, lakini kuwaona ndugu wakiwa
pamoja, kuwa mfano mzuri kwa familia zingine na kwa watoto wetu.
Tafadhali, jishushe, samehe na sahau, bado tunaweza kubadilisha hili
jambo. Kama nilisema chochote au kufanya chochote nilichokuumiza,
nisamehe. Na kwa mashabiki wetu wote wa ukweli, tafadhali tuombeeni.
Mungu awabariki wote.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...