• Home
  • About

LIFE STYLE | Wanawake huchepuka kwa sababu hizi...



Wapenzi wasomaji kumekuwa na manenomaneno kwamba, baadhi ya wanawake wamekuwa na mwanaume zaidi ya mmoja, lakini nimefanya utafiti na kubaini wanaosababisha tabia hiyo ya michepuko ni wanaume ambao wameingia nao kwenye uhusiano.

   
KWA NINI NASEMA HIVI?
Utakuta mwanamke alimpenda mwanaume fulani kwa sababu ya kufuata huduma na jinsi anavyomjali na kumheshimu ikiwa ni pamoja na kumjaza katika nafsi yake, pengine ndiyo anavyopenda au alikuwa havipati kutoka sehemu nyingine.
Lakini unakuta mwanaume anamkatisha tamaa mwanamke baada ya kuwa naye kwa muda mrefu. Sijui ni kumchoka au kitu gani!
WALICHONIAMBIA WANAWAKE
Nasema hivyo kwa sababu wanawake wengi wamenitumia malalamiko na kudai kuwa, wanaume wao kwa sasa wamewabadilikia. Walivyoanza mapenzi yalikuwa motomoto lakini sasa mambo ni tofauti. Hebu msikie huyu:
“Nakumbuka wakati nimeanza uhusiano na mpenzi wangu ilikuwa nikikohoa tu ananiuliza unataka nini mpenzi! Simu na meseji haziishi na kila sehemu tulikuwa pamoja. Lakini sasa hata nikimuomba kuongozana naye anasema yupo bize, sijui mapenzi yameisha au ubize umekuja sasa hivi!”
MANENO YANGU KWA WANAUME
Hivi wewe mwanaume unayemfanyia hivyo mwenzako na ulishamzoesha kuwa naye karibu kila wakati, unadhani akichepuka atakuwa amefanya vibaya?
Kumbuka kuwa, alizoea maisha hayo na wanawake wengi wamekuwa wakipenda kubembelezwa. Mwanamke anaweza asipende utajiri wako au muonekano wako lakini akakupenda jinsi unavyomjali na kumuonesha upendo.
SIKIA TENA
“Kutokana na kuzoea kuchati na mpenzi wangu ambaye kwa sasa hajibu SMS hata nikimtumia, nimejikuta nikiwa na mtu mwingine ninayechati naye ambaye huniondolea mawazo. Nimelazimika kufanya hivyo kwani nilizoea hivyo,” anasema msomaji mwingine.
NDIYO MAANA MUNGU AMEWEKA NDOA
Mwenyezi Mungu alipoweka sheria ya ndoa alikuwa na maana kubwa kwani hata mume akichoka vipi ni lazima afuate sheria za ndoa kwa vile ana wajibu wa kujua mwenzake amekula nini, amevaa nini, ana tatizo gani na unyumba ndiyo haswa! Hata akitoka atarudi tu.
KWENU MSIYOTAKA NDOA
Kwa wale msiotaka ndoa hili ni tatizo. Mtaendelea kuchepuka mpaka mwisho wa maisha yenu, kwani asiyekuwa na hili ana lile, wanaume wote ni sawa.
Hili liwe somo kwa wanawake wote, mwanaume si ndugu yako. Ni mwepesi kukubadilikia na kama ana mke ndo’ kabisa umeliwa bibi.Tafuta wako akuweke ndani la sivyo utahama vijiwe mwanzo mwisho. Je, kila mwanaume utamzalia? Watoto utawalea vipi?

Credit: Bongo61.com

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...