• Home
  • About

Hii ndio sababu ya Director Nisher ku step down...

 Muongozaji wa video ama director Nisher ameeleza jinsi alivyofanya kazi kupita kiasi ndani ya mwaka 2013/2014 hali iliyomsababisha kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali.

Nisher ambaye kwa sasa yupo mapumziko, amekiambia kipindi cha Mkasi cha EATV kuwa, hali hiyo ilisababisha familia yake imshauri apumzike.
nisher location
“Nilikuwa nafanya kazi sana kuanzia mwaka 2012, 2013 mpaka 2014 mpaka kuna kipindi nilizimia nikiwa naedit video. Nikaanguka chini next time naamka nakuta nipo hospitali nimetundukiwa drip naambiwa ulizimia. Kwa sasabu I was working too much ili kuprove watu wanachotaka,” alisema.
Aliongeza,”Kwa mfano sasa hivi sitoi tena kazi nipo break, this industry ina tendency ya kukufanya ujisikie, ujione yaani kuna wasanii wengi ambao wakishafaulu wanaanza kuwaangalia wenzao kama hawana kitu chochote. So nikaanza kuona kama naanza kufika hicho kipande na kama nakinusa hivi so nikawa mwepesi hivi kustep down.”

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...