Rapper mkongwe Juma Mchopanga a.k.a Jay Moe amesema kuwa mapokeo ya single
mpya anazotarajia kuanza kuzitoa hivi karibuni ndizo zitakazompa uhakika
wa lini atatoa album yake mpya.
Jay Moe ambaye amekaa muda mrefu bila kutoa nyimbo wala video,
amesema kuwa mwezi huu wa sita anatarajia kuachia single mpya pamoja na
video.
“Nadhani tutaanza kutoa singles, ndani ya huu mwezi wa sita tunaweza
kuanza kurelease single ya kwanza ya pili, video yake ukizingatia watu
wamekaa muda mrefu bila kuona video ya Jay Moe, kwahiyo nadhani hiyo
itakuwa nafasi nzuri sana kuweza kurudi.” Alisema Jay Moe kupitia E-Newz
ya EATV.
“Kwahiyo baada ya hapo respond ikiwa nzuri kurelease album ambayo
tayari unayo sio kazi, kazi ni kutoa singles watu wakazikubali tayari
kuinunua hiyo album.”
“Nadhani kwanza album itategemea na respond nzuri ambayo itatoka
kwenye singles ambazo ntaachia. Kuna nyimbo tatu, nne, tano kali sana
nimezirekodi kwenye nyimbo zaidi ya ishirini, kwahiyo tumepick zile kali
zile kila mtu akisikia anasema yeah hii hapa inaweza ikakurudisha
vizuri.” Alimaliza Jay Moe.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...