• Home
  • About

Diamond atajwa kuwania tuzo ya NEA nchini Nigeria mwaka huu...

  Diamond Platnumz kama anavyo fahamika ametajwa kuwania tuzo nyingine za Nigeria, ziitwazo Nigeria Entertainment Awards 2015 (NEA).
NEA
Majina ya wanaowania tuzo hizo yametangazwa jana, June 11 siku ambayo pia yalitangazwa majina ya wanaowania tuzo za MTV (MAMA) 2015 ambapo Diamond anashindania vipengele vitatu kwenye tuzo hizo.

  Katika tuzo za NEA Diamond anashindania kipengele kimoja cha African Artist of the Year (non-Nigerian) ambacho ni maalum kwa wasanii wasio Wanigeria.

Wasanii wengine wanaoshindania kipengele hicho ni Eddie Kenzo (Uganda) , SAUTI SOL (Kenya), Sarkodie (Ghana), na Stoneboy AKA Mzvee,.
Tuzo za NEA ambazo zinafanyika kwa mara ya kumi, zinatarajiwa kutolewa September 6, 2015 New York, Marekani.
Hii ndio orodha ya anao shinda nao..

African Artist of the Year (Non-Nigerian)
Eddie Kenzo
Diamond Platinum
SAUTI SOL
Sarkodie
Stoneboy
AKA
Mzvee

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...