Alikiba na Jacqueline Mengi wameungana na serikali ya Tanzania pamoja
na shirika la kimataifa la WildAid katika kampeni dhidi ya ujangili.
Mastaa hao pamoja ni miongoni mwa mabalozi wa kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo ‘Ujangili Unatuumiza Sote.’
Lengo la kampeni hiyo ni kukomesha biashara haramu ya wanyama pori
kwa kupungiza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyama hao kupitia
kampeni za uhamasishaji.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika kwenye hoteli ya Sea Cliff jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu, mabalozi wa China na Marekani, Alikiba na Jacqueline Mengi na
viongozi wa dini.
Wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni mwenyekiti mtendaji wa WildAid,
Peter Knights na mwenyekiti mtendaji wa African Wildlife Foundation,
Dr. Patrick Bergin.
Kampeni hiyo ina lengo la kukuza uelewa kwa wananchi wa Tanzania
kuhusu kukithiri kwa uwindaji haramu na kuongeza jitihada za kuwalinda
tembo na wanyama wengine wa porini.
Takwimu zinazonesha kuwa Tanzania imepoteza zaidi ya asilimia 60 ya tembo wake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Watu wengine maarufu duniani wanaotumika kwenye kampeni hiyo ni
pamoja na Prince William wa Uingereza, Jackie Chan na mchezaji wa zamani
wa kikapu wa China Yao Ming.
-------------------------------------------------------------------------------------------
Credit | bongo5.com
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...