Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali
ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’
ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata
vilema…“– Mbowe.
Tumeona
mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa
hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha
zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya
Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada
ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa
ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu
kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio
fedha za umma?“– Mbowe.
Kwa uzito
huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea
fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi
na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza
kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana
Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya
yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“
Ningeweza
nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya
kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa
Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na
mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa
yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa
uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Baada ya majibu hayo, Mbowe alipata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa Waziri Mkuu; “…Pamoja na kwamba jambo
hili litajitokeza baadaye katika mijadala ya leo, bado haiondoi ukweli
kwamba una wajibu wa kulijibu swali langu. Naomba kwa heshima sana
nikuulize tena kwa mara nyingine, taifa limepata fedheha kubwa sana kutokana na sakata hili, nchi nzima inasikiliza tatizo hili…“– Mbowe.
“…Una heshima kama kiongozi wa Serikali lakini heshima ambayo itakuwa imethibitishwa zaidi
kama utaamua kujiwajibisha mwenyewe ili kuweka heshima yako na heshima
ya Serikali, je kwa mara nyingine huoni ingekuwa vema kama basi utujibu
kama unafikiri bado zile fedha ni za umma kama hutaki ku-declare
kujiuzulu katika hatua ya sasa?”– Mbowe.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu amesema; “…Naomba
nirudie nilichosema, suala la kujiuzulu si jipya lakini maadam jambo
hili liko hapa Bungeni, unatanguliza hili jambo kwanini? Tungoje
tujadili tufikie mwisho halafu tutaamua…”– Mizengo Pinda.Sikiliza zaidi hapa..
CREDIT : Millardayo.com
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...