Rais mtawala wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameurejea uamuzi alioufanya miaka
mingi iliyopita wa kuwafukuza wakulima wa kizungu nchini humo, na sasa
amekaza kamba zaidi.
Mugabe ametoa tamko katika mkutano wa hadhara kuwa hawataki wakulima wa kizungu na kwamba ni lazima waondoke.
“Hatuwataki wakulima wazungu kumiliki mashamba yetu, lazima waondoke.”
Rais Mugabe anakaririwa.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu
waliosalia nchini humo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi
hiyo.
"hatuwataki wakulima wazungu, kumiliki mashamba yetu, lazima
waondoke,'' Mugabe aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara.
Rais Mugabe ameendelea kushikilia msimamo wa kuwapokonya ardhi
wazungu na kuwamilikisha raia wa nchi hiyo huku akitaka wazawa kutokuwa
wakarimu sana kwa wazungu kwa kuwa mashamba sio yao.
Mugabe mwenye umri wa miaka 90 ameiongoza Zimbabwe tangu ipate uhuru
mwaka 1980 na mwaka jana alishinda katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa
kupata asilimia 61 ya kura zote zilizopigwa.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...