Mwana mitindo na mrembo wa kimataifa aliyewahi kuvaa taji la Miss Tanzania, Happiness
Millen Magese ametoa machozi kwa uchungu wakati akisimulia kuhusu tatizo
la Endometriosis lililompelekea kuwa mgumba.
Millen Magese ameshindwa kuvumilia wakti akifanya mahojiano na Global
TV ambapo ameeleza kuwa alilazimika kufanya upasuaji mara 12 na
hatimaye kuondolewa kizazi.
“Nimeshafanyiwa upasuaji mara 12 na mirija yangu yote imeziba, upande
wangu mmoja wa ovary haufanyi kazi. Ile ndoto yote ya mimi kama
mwanamke kupata mtoto kwa njia ya kawaida imetoweka.” Amesema Happiness
kwa huzuni.
Ameeleza kua aliamua kuondoa kizazi ili baadae amuasili mtoto kwa
kuogopa kumuambukiza tatizo hilo mtoto ambaye angemzaa (endapo angezaa
mtoto wa kike).
Amesema tukio hilo ndilo lililomsababisha aanzishe taasisi ya kusaidia wanawake wengine ili wasipate tatizo kama lake.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...