Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewapokea rais wa
Israel, Shimon Pez na rais wa Palestina, Mahamoud Abbas katika makao
makuu ya kanisa hilo Vatican kwa lengo la kufanya maombi maalum ya
kuombea amani ya mashariki ya kati.
Walikutana na papa nje ya makaazi yake na baadae kuungana na kiongozi
wa kanisa la Ordhodoz, Partriarch Artholomew kwa hafla maalum.
Papa alizungumza katika hafula hiyo fupi:
“Kuleta amani kunahitji ujasiri mkubwa kuliko vita. Kunahitaji
ujasiri wa kusema ndio kwa mkutano na La kwa vita; ndio kwa mashauriano
na La kwa makabiliano; ndio kwa kuheshimu mikataba na La kwa uchokozi;
Ndio kwa ukweli na La kwa Uongo; kwa haya yote tunahitaji ujasiri na
nguvu moyoni.”
Maombi ya imani ya Kiislamu na imani ya Kikristo yatafanyika Vatican
ikiwa ni mara ya kwanza maombi na mafundisho ya Quran kufanyika hapo.
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...