• Home
  • About

Falcao kuzi kosa fainali za kombe la dunia Brazil

Heartbreak: Colombian striker Radamel Falcao will miss the World Cup in Brazil
Breaking the news: Falcao with manager Jose Pekerman at a press conference
 Falcao akiwa na kocha wake Jose Pekerman kwenye mmkutano na waandishi wa habari
Staying behind: Amaranto Perea (left), Luis Muriel (second left) and Falcao (right) were all left out

 MASHABIKI wa Colombia wamepagawa na taarifa kwamba nyota wao Radamel Falcao atazikosa fainali za kombe la dunia za mwaka huu nchini Brazil.

 Kocha wa timu ya Colombia, Jose Pekerman jana jumatatu alitangaza kikosi chake katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Buenos Aires, nchini Argentina.

Falcao alipata majeruhi kubwa ya goti akiwa katika majukumu ya kuitumikia klabu yake ya Monaco mwezi januari, na ameachwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambapo kocha wake amesema hatakuwa tayari.
Nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid  alisajiliwa kwa dau kubwa mno majira ya kiangazi mwaka jana, lakini kutokana na majeruhi aliyopata alikosa matumaini ya kulitumia taifa lake katika fainali za kombe la dunia mwaka huu.
Pekerman alisema wiki iliyopita kuwa atasubiri mpaka siku ya mwisho na dakika ya mwisho  ili kufanya maamuzi juu ya Falcao baada ya kuona anaimarika kidogo kidogo, huku akionana na madaktari wake, na mwisho wa siku, hapo jana alifanya maamuzi kinyume na maneno yake.
 
Kikosi cha wachezaji 23 wa Colombia hiki hapa
David Ospina (Nice), Faryd Mondragon (Deportivo Cali), Camilo Vargas (Santa Fe)
Camilo Zuniga (Napoli), Pablo Armero (Napoli), Cristian Zapata (AC Milan), Mario Yepes (Atalanta), Carlos Valdes (Philadelphia Union – on loan to San Lorenzo), Santiago Arias (PSV Eindhoven), Eder Alvarez-Balanta (River Plate)
James Rodriguez (Monaco), Abel Aguilar (Toulouse), Carlos Sanchez (Elche), Fredy Guarin (Inter Milan), Juan Fernando Quintero (Porto), Aldo Ramirez (Morelia), Alexander Mejia (Atletico Nacional), Victor Ibarbo (Cagliari), Juan Guillermo Cuadrado (Fiorentina)
Jackson Martinez (Porto), Teofilo Gutierrez (River Plate), Carlos Bacca (Sevilla), Adrian Ramos (Borussia Dortmund).

 Credit | Shafiidauda.com

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...