• Home
  • About

Six times two kuingia sokoni soon

Filamu ya Six times two imekamilika na inatarajia kutoka Tarehe 22. May. 2014, sinema hiyo ambayo imetengenezwa na mtayarishaji na mwigizaji wa filamu Zamo Chambo na kuwashirikisha wasanii nyota kama vile Jack Wolper, akiongelea sinema hiyo Zamo alisema.
 Six times two
Filamu hiyo iliyotengenezwa na Zamo Entertainment ya jijini Dar es Salaam, imesimamiwa na wataalamu waliobobea na kuifanya iwe sinema ya mfano kwa kazi nyingine, akiongea na FC Zamo alitamba kuwa toka aingia katika tasnia ya filamu amekuwa akitoa kazi zinazokubalika na wapenzi wa movie nchini.
“Ni kazi ambayo nimeifanya kwa ustadi mkubwa kabisa, ninatarajia kuwa wapenzi wa filamu Bongo watafurahia kuiona kazi inayoelimisha na kufundisha kwa jamii yetu,”anasema Zamo.

Filamu hiyo inasambazwa na kampuni ya kizalendo ya Yuneda Entertainment kila kitu kimekamilika, na itapatikana nchi nzima, kuanzia tarehe 22, mwezi wa tano mwaka huu siku ya Alhamisi. HAKIKISHA UNAPATA NAKALA HALISI YENYE STEMPU YA TRA, KUWA MZALENDO KWA KUNUNUA BIDHAA HALALI.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...