Msanii wa muziki tokea Chamber Squad anae fahamika kwa jina la Mez b ni mfuasi mzuri wa vitendo vya kauli ya Ben Pol alivyo imba kwenye nyimbo yake ya ‘Jikubali’ na anaamini kuwa yeye ndiye mkali zaidi kuliko wakali unao wa fikiria bongo nahata Africa Mashariki kiujumla.
Mez B ambaye hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaitwa ‘Shemeji’
amefunguka baada ya kuulizwa kuhusu alivyojipanga kurudi kwenye game na
kupenya katikati ya wasanii wapya wenye vipaji vya hali ya juu.
“Mimi kwanza nawapongeza wasanii wote kwa sababu wana vipaji
vizuri, ni changamoto nzuri. Kwa mimi Mez B na kwa mtu anaemfuatilia Mez
B, Mez B ni msanii mwenye kipaji cha kipekee sana, sijifananishi na
msanii yeyote Tanzania. Sisemi hivyo kama watu hawafanyi vizuri…watu
wanafanya vizuri. Lakini mimi naamini naimba kuliko msanii yeyote
Tanzania. Labda hata Afrika Mashariki.” Amesema Mez B.
Mwimbaji huyo ameeleza kuwa anaamini angeonekana zaidi kama kiwanda cha muziki Tanzania kingekuwa tofauti na kilivyo sasa.
“Kama game ingekuwa linaruhusu tufanye kweli muziki
international, sio huu muziki ambao wanahip hop huwa wanatutania wabana
pua. Kama game lingekuwa linaruhusu kweli tupige game, kweli tufanye
muziki wa kweli mimi naamini ningekuwa namba moja Tanzania kuwa na
muziki mzuri, kuwa na muziki ambao unaweza uka-sale hata nje kimataifa.” Ameeleza.
Amesema kwa sasa haoni kama kuna mabadiliko makubwa yaliyofanyika
kwenye muziki kiasi cha kuufanya muziki alioufanya zamani kuwa ni muziki
uliopitwa na wakati.
“Kilichobadilika sasa hivi labda ni temple ya muziki imebadilika,
lakini pia fitina zilizopo kwenye muziki, kwa maana kwamba muziki sasa
hivi lazima uwe na uwezo (kifedha) ili uweze kuufanya muziki wako
vizuri. Lakini kwa uwezo wa uimbaji kusema ukweli mimi bado sijaona mtu
yeyote anaenitishia amani Tanzania…samahani kwa kusema hivyo lakini..”
Katika hatua nyingine Mez B amesema baada ya kuachia wimbo wa ‘Shemeji’ ameamua kufanya
kampeni ya kuhamasisha watu watulie katika ndoa zao na kuachana na
michepuko na ataifanya katika mikoa 5 tofauti.
Ataendesha kampeni hiyo katika mikoa ya Dodoma, Mtwara, Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam.
Credit | Timesfm
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...