Mohammed Dewji ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited amefanya mahojiano na BBC kuhusu uwekezaji wa ndani ya
nchi na jinsi uchumi wa Tanzania unavyokua.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi wa Tanzania unaongezeka kwa
kiwango fulani na hivyo kampuni ya Mohammed Dewji pia ni moja kati ya
makampuni yanayofaidika zaidi na ongezeko hilo.
“Nchi kwa ujumla inafanya vizuri sana, tumeendelea kukua kiuchumi kwa
asilimia 7 na tuko kati ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakua
haraka zaidi.” Amesema Mohammed Dewji.
Ameeleza kuwa kuna ongezeko la pato la Tanzania kutoka dola milioni
30 mwaka 1999 hadi dola bilioni 1.1 na kwamba hata kampuni yake inakua
zaidi kwa kuwa watu wanavyozidi kuongeza pato ndivyo uwezo wao wa
kununua bidhaa unavyoongezeka.
Amesema kuwa sasa hivi wanaendesha kampeni ya kununua vitu vya
Tanzania ‘to buy Tanzanian’ na kwamba hiyo inawezekana zaidi endapo
makampuni yatatoa bidhaa bora zaidi na kuweka bei inayomudu ushindani,
watanzania watanunua zaidi bidhaa za kwao.
Ameongelea pia kuhusu umoja wa nchi za Afrika Mashariki na kueleza
kuwa kiuchumi utasaidia sana lakini watanzania wengi walikuwa bado
wanauoga kuhusu kiwango cha watanzania ambao wamepata elimu kwa
kulinganisha na nchi nyingine wanachama.
BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA ZAIDI...
http://www.bbc.com/news/world-africa-26692518
Post a Comment
LEAVE YOUR COMENT HERE...