• Home
  • About

LIFE STYLE : Wapenzi kuchokana haraka...



Baadhi yetu hatuwezi kukubali,  ukweli kuwa mapenzi ndiyo yanaendesha dunia, kwani hata Ali Kiba ana kibao chake kinachoukubali ukweli huu kwamba mapenzi yana-run dunia.
black-couple-bed
Katika baadhi ya mahusiano ya kimapenzi, wapo wanaochokana haraka kiasi cha kumshangaza mmoja wa wahusika, awe mwanaume au mwanamke, ingawa uzoefu unaonyesha akina baba wengi ndiyo wenye tabia ya kukinai mapema.
Wanaanza kwa kasi na nguvu kubwa, wakipiga simu kila baada ya muda mfupi na sms kila dakika, lakini wakishafanikiwa kukutana kimwili na mwenzake mara moja au mbili, taratibu ukaribu unaanza kuota mbawa, mithili ya mapenzi ya miaka sita au saba iliyopita.
Hali hii inakuwa zaidi kwa wanaume, kwani ikishatokea wamekutana na mwenza wake zaidi ya mara moja, wanaanza kupoteza spidi ya mwanzo, huku baadhi yao wakileta dharau na sababu zisizo maana katika kuhalalisha tabia yao mpya.
Hivi karibuni mwanamke mmoja msomaji wa safu hii, alinilalamikia juu ya tabia ya mpenzi wake aliyekuwa akimsumbua sana mwanzoni, lakini sasa mwanaume amebadilika kabisa baada ya kukutana naye mara tatu faragha.
Nilijitahidi kumpatia ushauri ambao naamini utamsaidia, lakini hapo hapo nikapata wazo la kuandika mada hii hapa nikiamini itawasaidia wengi pia kwa kuzingatia hali hii wanakutana nayo wanawake wengi. Zifuatazo zaweza kuwa sababu zinazochangia hali ya mwanaume kupotea haraka mara baada ya kufanikiwa kukutana kimwili na mwenza wake.

HANA MAPENZI YA DHATI
Kuwa makini, siyo kila anayetamka neno I love you anamaanisha. Wengi wanatawaliwa na tamaa ya kingono tu na hawana mapenzi ya dhati. Na wengi wa wanaume wapya unaokutana nao, wana wapenzi wao tayari.
Ndiyo maana wanaume wengi wa aina hii, wanakimbilia kutaka kukutana kimwili na ili wafanikiwe katika hilo, watatumia kila aina ya mbinu wanazozijua. Unapokutana na wa aina hii, jipange, usije kutafuta wa kumlaumu. Kwa ujumla, akina kaka wa aina hii ni wenye kuongozwa na uchu wa kimwili.
UJUZI FARAGHA
Sayansi na teknolojia zimeleta mambo mengi. Siku hizi watu wanaangalia mitindo ya mapenzi mitandaoni. Wanatamani kukutana na wanachokiona kutoka kwa wapenzi wao. Hivyo wanapokosa, nao hupoteza hamu.
200910-omag-argument-949x534
KUTOTIMIA KWA MATARAJIO
Wapo wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu wakitegemea kufaidika kwa kitu flani, kama vile mabadiliko ya maisha yao na kadhalika, hivyo inapokuwa tofauti, hujiondoa mapema.
MAZOEA
Tatizo hili mara nyingi linawakuta akina dada. Wakishakuwa na mtu kwa muda mrefu huchukulia kuwa ni mazoea na hivyo kufanya wanavyotaka bila kujua kuwa wanawaudhi wenza wao, ambao ili kujiweka sawa kiakili huamua kusaliti na au kusababisha dharau baina yao.
KUTOJALI
Hii zaidi ipo kwa wanaume, pale mwanzo walikuwa wakijali kwa kusikiliza na kutimiza shida za wenza wao, lakini baada ya kupata walichohitaji, hawana tena ‘mzuka’. Jambo hili huwakera wenza wao na kujikuta wakiamua kukata mawasiliano mapema.Ushauri ni kwa wote, wake kwa waume, kila mmoja kuwa chachu ya ustawi wa penzi, badala ya kusubiri kufanyiwa unachotaka!
MAZINGIRA
Hii ni moja ya sababu ambayo pia inasababisha wapenzi wengi kuchokana haraka. Utakuta wapenzi wamezoea kukutana faragha chumbani tu hakuna hata siku moja ambayo wanabadilisha mazingira
Wapenzi wanatakiwa kubadilisha mazingira kwani wasipofanya hivyo, hata akili huwa inachoka na hii haimaanishi labda muende hotelini, inawezekana hamna uwezo huo, basi fanyeni mabadiliko ya mazingira hukohuko nyumbani kwenu, yaani mnabadilisha maeneo, kama leo mlizungumza mkiwa sebuleni, basi kesho mfanye hivyo mkiwa kwenye kochi na siku nyingine mnaweza kushusha godoro  chini!
MAWASILIANO
Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika mapenzi. Katika ulimwengu wa leo hakuna mapenzi kama hakuna mawasiliano.Hapa ninazungumzia wapenzi kuwasiliana kama kupigiana simu, kutumiana meseji  za kuulizana umeshindaje, umekula, kazi na mengine mengi, hii ni kinga tosha ya kutochokana haraka, hivyo hata kama uko bize kiasi gani jitahidi kuwasiliana na umpendaye.
Wapo wapenzi ambao wanapitisha hata siku mbili au tatu bila kuwasiliana na wenza wao wakati mwanzoni mwa penzi lao haikuwa hivyo, walikuwa wanatumiana meseji au kupigiana simu kila wakati lakini siku zinavyokwenda ndivyo mawasiliano yanakuwa hafifu au unakuta mmoja yaani mwanamke au mwanaume ndiye anayejitoa kila wakati kujitahidi kuwasiliana na mwenzake, lakini mwisho anachoka na penzi linaishia hapo maana hakuna thamani au wanajikuta wanatafutana pale mmoja anapokuwa na uhitaji wa kimwili, haya siyo mapenzi.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...