• Home
  • About

Hivi ndivyo Soko la Karume jijini Dar lilivyo teketea usiku wa kuamkia leo...

  Moto mkubwa ume teketeza soko kubwa la mitumba la jijini Dar Karume, Soko hilo lina ripotiwa kuanza ku teketea kuanzia saa 4Usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa mashuhuda nikua wali jaribu kuuzima moto huo kuanzia muda huo bila kufanikiwa . Zima moto waliweza kufika na kuuzuia moto huo ulio kua ume fika karibu na kiwanda cha breweries, Hauku sababisha madhara yeyote kwa nyumba za jirani na soko hilo.

Mwenyekiti wa soko hilo, Jumanne Song’o ameeleza kuwa asilimia 85 ya soko hilo ndiyo iliyoteketea kabisa na kwamba ni wafanyabiashara 3,000 waliokuwa wakifanya shughuli zao kisheria lakini kwa sasa idadi yao ni zaidi ya 10,000.

Ameeleza kuwa moto huo umesababisha hasara kubwa na athari kubwa kwa wafanyabiashara hao kwa kuwa wengi wao hutumia fedha za mikopo kuendesha biashara.
Nae Meya wa Ilala, Jerry Slaa aliyefika katika eneo la tukio amewataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu na kwamba halmashauri itashirikiana nao kwa hali na mali kufahamu chanzo cha moto huo.
Mheshimiwa Slaa amesisitiza kuwa wafanyabiashara hao wapo katika soko hilo kisheria na kwamba atahakikisha wanaendelea kuwepo.
 Moto mkubwa
Akieleza kuhusu athari za mikopo walizopata wafanyabiashara hao, Mheshimiwa Slaa amesema watafanya kikao cha dharua leo mchana kitakachowajumuisha viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Ilala ili tathimini ya thamani ya mali iliyoteketea pamoja kujadili mengine muhimu ya kuwasaidia wafanyabiashara hao wanaoishi kwa kutegemea mikopo.
Mabaki ya baadhi ya vitu yakiwa yana endelea teketea
Shukhuli za kuzima moto ziki endelea.

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...