• Home
  • About

George tyson kuagwa kesho leaders naku pelekwa nchini kwao kwa maziko..

Marehemu George Tyson aliye kua muongozaji wa filamu na vipindi vya Television mwili wake  utaagwa kesho (June3) katika viwanja vya leaders Club, Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwenda kwao nchini Kenya kwa maziko.

“Tunashukuru Mungu mwili wa George Tyson umewasili jana Dar es salaam ukitokea mkoani Morogoro na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Kairuki, kumuaga marehemu itakuwa Leaders Club siku ya Jumanne na baada ya kuuaga mwili utasafirishwa Kenya kwa mazishi.” Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere ameiambia Bongo5.
 Marehemu George Tyson Otieno, alifariki katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Gairo, Morogoro alipokuwa akitokea Dodoma na timu ya The Mboni Show kutoa msaada wa madawati kwa shule moja ya msingi na walikuwa njiani wakirudi jijini Dar es Salaam.
 Katika gari hilo alilokuwemo marehemu Tyson na watu wengine nane na yeye pekee ndiye aliyepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa..

Post a Comment

LEAVE YOUR COMENT HERE...